Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la AhlulBayt (as) -ABNA- sifa ya “Mashujaa wa kupinga dhuluma na mapambano” imeambatana na familia za Kisayyid (wana wa Mtume) kwa zaidi ya miaka 1,400. Historia ya Uislamu haijawahi kuwa bila ya upinzani kutoka kwa kizazi cha Mtume (saw), waliopambana kwa njia mbalimbali dhidi ya maadui wa dini na ukweli.
Miongoni mwa mifano mashuhuri ni harakati na vuguvugu za kijihadi na kimapinduzi zilizoongozwa na watoto na wajukuu wa Imam Sajjad (as), hususan Zayd bin Ali (as), ambaye alikuwa mwana wa Imam Sajjad (as), na harakati zilizofuata baada ya yeye. Harakati hizi mara nyingi zilikuwa na uungwaji mkono wa wazi au wa siri kutoka kwa Maimamu wa AhlulBayt (as).
Familia ya Khamenei wanatambulika kama kizazi cha ishirini na tisa (29) kutoka kwa Sadaat Afṭasi, kizazi kinachotokana na Hasan al-Afṭas, mwana wa Ali al-Asghar, mwana wa Imam Ali bin Husayn Zainul-Abidin (as). Katika familia hii, walikuwepo wanazuoni na wapiganaji mashuhuri, miongoni mwao ni:
1- Abul-Hasan Ali Dinawari (alizaliwa mwaka 189 Hijria): aliyekuwa mwakilishi wa Imam Jawad (as) katika maeneo ya Dinawar (eneo la milima ya Zagros na mkoa wa sasa wa Kermanshah).
2- Sayyid Ahmad bin Muhammad al-Mada’ini: babu mkubwa wa familia ya Khamenei. Alikuwa mwanazuoni mpambanaji aliyehamia Hizāwah (katika mkoa wa sasa wa Markazi) ili kuepuka dhuluma za utawala wa Abbasiyya, na aliuawa shahidi mwaka 360 Hijria wakati wa Sala ya usiku. Kaburi lake bado linajulikana, na Kiongozi Mkuu wa Iran (Ayatollah Khamenei) aliliendea kwa ziara akisema: "Ninajivunia kwamba huyu mtu mashuhuri ni babu yangu."
Katika ukoo huu, mamia ya watu walijihusisha na dini na siasa. Ingawa makala hii hailengi kuelezea historia ya kila mmoja wao, inaonesha mizizi ya kidini na kisiasa ya familia hiyo.
Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu (Ayatollah Khamenei), katika hotuba yake ya tarehe 27 Aban 1379 (Sawia na 17 Novemba 2000) alipokutana na watu wa Tafresh, alieleza kuhusu ukoo wake akimtaja Sayyid Qutbuddin kama babu yake wa kumi. Alieleza kuwa ukoo huu una matawi mawili:
-
Tawi la Sayyid Zohiruddin na Sayyid Fakhruddin (anayeitwa Mir Fakhra), ambao ndio ukoo wa Khamenei.
-
Tawi lingine ni ukoo wa Qa’im Maqam Farahani, unaojumuisha watu mashuhuri kama Mirza Issa na Mirza Abu al-Qasim Qa’im Maqam Farahani.
Alieleza kuwa ukoo wao ulihamia kutoka Tafresh hadi Khāmeneh, kisha kwenda Tabriz, na hatimaye Mashhad kupitia kwa Sayyid Muhammad, babu yake aliyekuwa kijana aliyetoka Tafresh kwenda Azerbaijan, na baadaye kuishi Khāmeneh.
Sehemu zijazo za makala zitaangazia historia ya karibuni ya familia ya Khamenei:
1- Ushiriki wao katika kupinga udikteta wa kifalme wa Qajar,
2- Jinsi walivyohusika katika mapinduzi ya katiba (Mashruteh),
3- Nafasi ya wanazuoni wa familia hiyo wakati wa utawala wa Reza Shah na Muhammad Reza Pahlavi.
Vyanzo vya makala:
-
Ensiklopedya ya Maeneo Matakatifu
-
Kitabu cha Maelfu ya Makaburi ya Iran (هزار مزار ایران)
Your Comment